Yanga Yamuongezea Mkataba Kibwana Shomari

Uongozi wa klabu ya Yanga SC, umemuongeza mkataba wa miaka miwili beki wao wa kulia, Kibwana Shomari kuendelea kuitumikia klabu hiyo, mkatab huo utadumu hadi mwaka 2026.

Yanga Yamuongezea Mkataba Kibwana Shomari

Kibwana ambaye ameitumikia Yanga kwa miaka mitatu tangu ametua akitokea Mtibwa Sugar, ataendelea kubaki zaidi ndani ya timu hiyo ya Jangwani kwa miaka mingine miwili.

Beki huyo ambaye ametwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA) anaendelea kupambania nafasi mbele ya Kouassi Attohoula Yao ambaye amekuwa panga pangua katika kikosi cha kwanza tangu ametua akitokea ASEC Mimosas.

Yanga Yamuongezea Mkataba Kibwana Shomari

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimefichua kuwa lilikuwa ni suala la muda kwa beki huyo kuongeza mkataba kutokana na uwezo aliouonyesha tangu ametua akitokea Mtibwa Sugar.

“Hatuwezi tukawa na beki mmoja wakati tuna mashindano mengi ya ndani na nje hivyo kuhusu kumuongeza mkataba Kibwana lilikuwa ni suala la muda tu sasa mambo yamekamilika,” kilisema chanzo hicho.

Hadi sasa, mastaa walioongezwa mikataba Yanga ni Djigui Diarra, Farid Mussa, Abuutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto, Jonas Mkude na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Yanga Yamuongezea Mkataba Kibwana Shomari

Huku klabu hiyo ikiwa imewatambulisha kundini wachezaji wanne hadi sasa, Kiungo Clatous Chama aliyetoka Simba, Prince Dube mshambuliaji alikuwa ni mchezaji huru akitokea Azam FC, Chadrack Boka kutoka FC Lupopo ya DR Congo ni beki wa kushoto, halafu kuna Mlinda mlango wa Ihefu Abubakar Khomeiny.

Acha ujumbe