Yanga Yapanga Kumsajili Erick Mwijage Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji

Licha ya tayari kuwatambulisha nyota wapya wanne, Juma Abushiri kutoka Fountain Gate FC pamoja na Mohamed Mussa, Abdulnasri Muhamed na Hussein Mihambo kutoka Mashujaa FC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wanaendelea na harakati za kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu wa 2026/27.

Yanga Yapanga Kumsajili Erick Mwijage Kuimarisha Safu ya UshambuliajiTaarifa zinaeleza kuwa Yanga imefikia hatua nzur  i katika mazungumzo ya kumsajili winga wa KMC FC, Erick Mwijage, ambaye ameonyesha kiwango bora katika misimu ya hivi karibuni. Inadaiwa kuwa mchezaji huyo amekubaliana kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo.

ligi kuu tanzania, nbc premier league, ligi kuu bara, odds za kubeti ligi kuu NBC, mechi za ligi kuu Tanzania, ligi kuu ya NBC,

Mwijage anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam muda wowote ili kukamilisha hatua za mwisho za usajili, zikiwemo vipimo vya afya, upigaji picha rasmi na kukamilisha taratibu zote za kimkataba kabla ya kutangazwa rasmi na klabu.

Yanga Yapanga Kumsajili Erick Mwijage Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji“Kila usajili ambao sisi tunaufanya unatokana na ripoti ya benchi la ufundi, mipango na mikakati ya kuhakikisha tunaendelea kuimarisha kikosi na kulinda hadhi ya timu yetu,” alisema msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe.

Yanga Yapanga Kumsajili Erick Mwijage Kuimarisha Safu ya UshambuliajiKiwango alichokionyesha Erick Mwijage akiwa KMC FC, pamoja na mchango wake mkubwa wakati akiichezea Kagera Sugar, kimevutia benchi la ufundi la Yanga. Endapo usajili huo utakamilika rasmi, utakuwa sehemu ya mkakati wa klabu hiyo wa kujenga kikosi imara kitakachowania mataji ya ndani na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.