UONGOZI wa Yanga Pamoja na benchi la ufundi chini ya kocha, Miguel Gamond kwa sasa wanapiga hesabu za mechi tatu ambazo zipo mbele yao za ligi kuu ambazo ni sawa na dakika 270 za moto kulingana na timu ambazo wanakwenda kukutana nazo.
Yanga katika mechi tatu zijazo za ligi kuu wanatarajiwa kukutana na Azam FC, Singida Fountain kisha dhidi ya Simba.
Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wao kwa sasa wanaweka mkakati mzito wa kuhakikisha wanazoa pointi kwa kila mpinzani ambaye anakuja mbele kupambana nao na kuhakikisha kuwa wanapata matokeo mazuri.“Kwa sasa mpango wetu mkubwa ni kuhakikisha tunavuna pointi katika kila mchezo ambao upo mbele yetu, tunafahamu kuwa tuna ratiba ya michezo mitatu migumu mbele yetu, lakini ni lazima tujiandae kucheza na timu yoyote na kukabiliana naye na kisha kuhitaji matokeo mazuri.
“Tumeweka malengo yetu sisi kama timu msimu huu kuona kuwa tunayafikia malengo yetu, viongozi wetu, wachezaji na benchi la ufundi wote wanafahamu tupo tayari kutimiza wajibu wetu, ili kuhakikisha kila upande unakuwa sehemu ya kutimiza malengo yetu,” alisema kiongozi huyo.
TUMEONA baada ya makundi kupangwa na kila mmoja kuwajua wapinzani wake mambo yamekuwa mengi. Huyu anasema kundi hili gumu lile jepesi.
Haya ni maneno ambayo yatakuwa yanawapa ugumu wachezaji kujua wapo kundi lipi. Kila kundi lina timu bora ndio maana zimetinga hatua ya makundi.
Kuanza kubeba matokeo wakati huu na kujipeleka hatua ya robo fainali anguko linakuja. Hakuna timu iliyopita kwa bahati mbaya kila timu ilikuwa na mipango.Ile mipango iliyopangwa kwenye hatua za mwanzo inapaswa kuwa endelevu. Muda uliopo kwa sasa ni kuwekeza nguvu kubwa kwenye maandalizi.
Tambo za Yanga na Simba hazikosekani lakini ukweli utabaki palepale kwamba sio Simba wala Yanga mwenye uhakika wa kutinga hatua ya robo fainali.
Ili utinge robo fainali ni lazima upate matokeo na hesabu huku ni pointi. Kupata pointi sio jambo jepesi maandalizi ni sasa kuelekea kwenye mashindano hayo makubwa.
Kelele na porojo hazina nguvu ya kuleta matokeo na timu kutinga hatua ya makundi. Kukwama kupanga mipango mizuri sasa ni muda wa kutengeneza anguko kesho.
Wakati ni sasa kuendelea kufanya maandalizi mazuri kwenye mechi za kimataifa. Hakuna muda wa kupoteza na kuanza kutamba kwamba timu itapenya kwa kuwa ina wapinzani dhaifu.
Kila mmoja anatafuta pa kutokea hata wale ambao mnawaona ni wepesi na wao pia wanawaona sehemu watakayokomba pointi ni kwenu.