Yanga Yapigwa Faini ya Milioni 30, Walter Harson Afungiwa Michezo Mitatu

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa maamuzi mbalimbali kufuatia matukio yaliyojitokeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC na Yanga uliochezwa Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam.

Yanga Yapigwa Faini ya Milioni 30, Walter Harson Afungiwa Michezo MitatuMaamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika Mei 9, 2026 baada ya kupitia ripoti na mwenendo wa mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika hatua ya kwanza, klabu ya Yanga imepewa onyo kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili uwanjani kuelekea mchezo huo. Taarifa zinaeleza kuwa timu hiyo iliwasili saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa chini ya Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu.

Yanga Yapigwa Faini ya Milioni 30, Walter Harson Afungiwa Michezo Mitatu

Aidha, Yanga imepigwa faini ya Shilingi milioni 30 baada ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia ndani ya uwanja huo. Badala yake, walitumia nyumba iliyopo nje ya uwanja upande wa pili wa barabara, jambo lililotajwa kuwa ni kinyume na Kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Yanga Yapigwa Faini ya Milioni 30, Walter Harson Afungiwa Michezo MitatuKamati hiyo pia imemchukulia hatua Meneja wa Yanga, Walter Harson, kwa kumfungia michezo mitatu pamoja na kumtoza faini y a Shilingi milioni moja. Adhabu hiyo imekuja baada ya meneja huyo kukutwa na kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba, Clatous Chama, wakati wa mchezo huo.

Kwa upande mwingine, shabiki wa Yanga aliyetambulika kwa jina la Mohamed Ally Mposo amefungiwa kuingia viwanjani kwa muda wa miezi 12. TPLB imesema shabiki huyo aliingia kwenye eneo la kuchezea wakati wa mapumziko na kumwaga vimiminika vilivyotafsiriwa kuwa ni sehemu ya imani za kishirikina.

Yanga Yapigwa Faini ya Milioni 30, Walter Harson Afungiwa Michezo MitatuKamati ya TPLB imeeleza kuwa hatua hizo zimechukuliwa kwa mujibu wa kanuni mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa lengo la kuhakikisha nidhamu, usalama na uendeshaji wa ligi vinaendelea kuzingatiwa katika michezo yote ya msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.