Yanga Yapigwa Faini

Klabu ya Yanga ambayo makao yake yapo Jangwani imepigwa Faini ya shilingi Milioni tano (500,0000) na Shirikisho la Mpira wa Soka Tanzania(TFF)  kwa kosa la kuingia chumba cha kuvalia nguo kwa kutumia mlango ambao sio rasmi kuelekea mchezo wao wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba.

 

Yanga Yapigwa Faini

Mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa tarehe 23 ya mwezi Oktoba na kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, huku Yanga wakisawazisha bao hilo kwa faulo ambayo ilipigwa moja moja na Aziz Ki.

Simba ndio walitangulia kufunga bao katika dakika za mapema sana kupitia kwa mchezaji wao Okrah lakini wakashindwa kutumia nafasi nyingine nyingi walizopata na kufanya mchezo kumalizika kwa sare.

Yanga Yapigwa Faini

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni 41:5(5,4) ya Ligi kuu kuhusu taratibu za michezo.

Yanga ndio vinara wa Ligi kuu ya NBC na kesho watakuwa dimbani huko Tunisia kucheza mchezo wa marudiano wa michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika  dhidi ya Club Africain baada ya mchezo wa kwanza kutoa sare ya bila kwa bila.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

Acha ujumbe