Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mtoano wa michuano ya Shirikisho barani Afrika dhidi ya Club Africain.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Novemba 9 mwaka huu ambapo ule wa awali uliopigwa Jijini Dar ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

yanga, Yanga Yasepa Tunisia, Meridianbet

Yanga ili waweze kuvuka katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Shirikisho wanapaswa kushinda au kutoa sare yeyote.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema: “Tumeumizwa na matokeo yaliyopita ya suluhu na hakuna mtu yeyote ambaye amejiandaa nayo.

“Tunawaomba wana Yanga kuwa wamoja na kuisapoti timu yetu tunaamini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye dakika 90 za mchezo wa marudiano kule Tunisia.

“Kwenye mpira lolote linawezekana tumefanya vibaya kwenye mchezo wa nyumbani kwa kutoka suluhu lakini tutaenda kupambana kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa