Kocha wa Yanga SC, Abdi Hamid Moallin, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaochezwa Juni 24, 2026, akieleza kuwa kila mechi iliyosalia kwa timu hiyo ni sawa na fainali katika mbio za kutetea ubingwa wa ligi hiyo.
“Kila mchezo kwetu ni fainali. Ushindani wa ligi msimu huu ni mkubwa sana na katika hatua hizi za mwisho hakuna nafasi ya kupoteza alama kama tunataka kufikia malengo yetu,” alisema Moallin wakati akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo huo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa wachezaji, beki wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’, amesema idadi ndogo ya mechi zilizosalia kabla ya msimu kumalizika imeongeza ari kwa kikosi hicho kupambana kwa nguvu zaidi katika kila mchezo.
Wakati huo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kassim Liogope, amesema timu yake imekamilisha maandalizi ya mchezo huo na ipo tayari kukabiliana na Yanga katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. “Sisi kama Azam, hizi ni aina ya mechi tunazozipenda. Wachezaji wako tayari na wanaelewa umuhimu wa mchezo huu,” alisema Liogope.
Nahodha wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda, amesema ushindi katika mchezo huo utategemea nidhamu ya wachezaji kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, akisisitiza kuwa timu itakayotekeleza mpango wake wa mchezo kwa ufanisi zaidi ndiyo itakayokuwa na nafasi kubwa ya kuondoka na pointi tatu muhimu.


