Klabu ya Yanga imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya klabu ya Asas ya nchini Djibout.
Katika mchezo uliopigwa katika dimba la Chamazi jijini Dar-es-salaam jioni ya leo klabu ya Yanga imeweza kupiga hatua moja mbele katika kuelekea katika mchezo wa pili ambao kama watashinda tena au kutoka sare basi watakua wamefanikiwa kwenda hatua nyingine.Alikua Stefane Aziz Ki ambaye aliwapa bao la uongozi wananchi katika dimba la Chamazi leo, Huku pia akiwa moja ya wachezaji bora kabisa katika mchezo wa leo akicheza kwenye ubora wa hali ya juu.
Mchezo huo ulienda mapumziko Wananchi wakiwa mbele kwa bao moja kwa bila ambalo liliwekwa kimiani na Aziz Ki lakini pia wakicheza mpira mzuri na wenye kuvutia.Wananchi walifanikiwa kupata bao la pili la mchezo kupitia kwa Kenedy Musonda ambalo ndio lilikua bao la mwisho katika mchezo huo pia, Baada ya mchezo wa leo Yanga wanajiweka kwenye nafasi nzuri ya kucheza raundi ya pili ya ligi ya mabingwa Afrika ambayo ndio inaweza kuwapeleka hatua ya makundi.