Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer aeleza kwamba anatamani na kuamini kwamba timu yake itafika fainali ya Europa League na kuchukua kombe hilo.

Manchester United walikuwa mwa miongoni mwa timu nne zilizotinga nusu fainali ya kombe la Europa, huku wakiwa pamoja na Arsenal kutoka EPL, Villareal kutoka La Liga and As Roma kutoka kule Serie A.

Magoli ya Manchester United katika mkondo wa kwanza yaliyofungwa na Marcus Rashford na Edinson Cavani yaliwaandalia mazingira mazuri United kusogelea nusu fainali. Mechi ya jana usiku ilikamilika kwa United kushinda magoli mawili, moja toka kwa Cavani na moja la kujifunga la Vallejo. Na kufanya jumla ya magoli kuwa 4-0.

Ole atamani ubingwa Europa

United watakutana na As Roma katika nusu fainali ya michuano hiyo tarehe 29 mwezi wa nne. Mechi hii inakumbusha mechi ya mwisho ambapo timu hizi zilikutana mwaka 2007 na Manchester United kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 8-3 kwa mikondo yote miwili ya nusu fainali ya UEFA Champions League. Katika mechi hiyo pia Solskjaer alikuwa miongoni wa wachezaji walioisaidia United.

Katika mechi hizo mbili, Man United walianza kupoteza 2-1 wakiwa ugenini, lakini walipofika old Trafford wakapindua matokeo na kushinda goli 7-1. Hii pia ilikuwa ndo mechi iliyomtambulisha Ronaldo kwenye kufunga kwenya UEFA Champions League ambaye alifunga magoli mawili.

Ole atamani ubingwa Europa

“Leo tumecheza vizuri sana, na kwa nidhamu kubwa. Tuna nafasi ya kufika fainali na ni lazima tufanye hivyo. Nimeona kila mchezaji anatamani hilo na tutafika fainali licha ya kukutana na timu kubwa” alisema Ole.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

Solskjaer, Solskjaer Atazamia Kuchukua Ubingwa wa Europa!, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa