Klabu ya Tottenham Hotspurs imethibitisha mshambuliaji wake Hueng-Ming Son, amesaini mkataba mpya wa miaka minne zaidi mpaka 2025.

Mchakato wa mkataba mpya kwa mchezaji huyu ulianza toka Juni,2021 na baada ya mchakato wa kupata kocha mpya sambamba na Mkurugenzi wa michezo wa Spurs kumalizika, hatimaye zoezi hili limehitimishwa rasmi.

Fabio Paratici ameshirikiana vyema na Daniel Levy katika kuhakikisha Son anabaki Spurs na wamefanikiwa kumpatia kandarasi mpya ya miaka minne.

“Hakukua na maamuzi. Ilikuwa ni rahisi tu. Ninafuraha kuwa hapa na ninasubiri kwa hamu kuwaona mashabiki kwa mara nyingine” alisema mchezaji huyo ambaye ameshafunga magoli 107 kati ya michezo 280.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa