Nyota wa Tottenham Son Heung-min ameripotiwa kurejea London baada ya kutumikia jeshi la Korea Kusini. Staa huyu alitumikia jeshi kwa mda wa wiki tatu baada ya nafuu kutokana na mafanikio yake kwenye Asian Games 2018.

Mshambuliaji huyu wa Spurs amerejea London wakati kukiwa na maandalizi ya kurejea mazoezini tayari kuisubiri ligi ianze. Baada ya kumaliza mafunzo yake ya jeshi kwa mujibu wa sheria alikaa kwa mda Seoul.

Son Arejea London Baada ya Kutumikia Jeshi!

Son alifanya vyema katika mafunzo yake ya jeshi na kuibuka kuwa miungoni mwa watu watano waliofanya vyema zaidi kikosini.

Amerejea London Jumamosi, na hatalazimika kukaa karantini peke yake labda ikiwa atapimwa na kupatikana na maambukizi ya corona. Vinginevyo, ataruhusiwa kuendelea na mazoezi pindi watakapoaanza kufanya pamoja kama timu.

Son Arejea London Baada ya Kutumikia Jeshi!
Son Heung-min

Likizo ya lazima ya Corona imekuwa kama nafuu kwa Son kwa upande mwingine ambaye ameweza kupona mkono wake uliovunjika, ambao ungemlazimu kukaa nje ya dimba kwa mda mrefu, pia likizo hii imempa nafasi ya kushiriki mafunzo ya jeshi bila kuathiri sana kuitumikia klabu yake ya Tottenham.

37 MAONI

  1. Miaka kadhaa ilikuwa lazima kwetu kujiunga mgambo baada ya kumaliza form six. Son ametukumbusha kuheshimu taratibu za nchi yako # Meridianbettz

  2. Ni jambo jema na la kumshukuru sana mungu kwake kwa kuwa amemaliza salama na kurudi akiwa na kazi yake nzuri.

  3. kama mwanzo alikaza vile itakuaje mwishon mwa msimu huu? son nadhani atakua wa moto zaidi ukilinganisha na wachezaji wengine ambao walikua karantin

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa