Kiungo mshambuliaji wa Hispania na klabu ya FC Barcelona, Lamine Yamal, ameanza rasmi mazoezi binafsi ya uwanjani pamoja na gym ikiwa ni sehemu ya hatua zake za kurejea kikosini baada ya kusumbuliwa na majeraha yaliyomuweka nje kwa muda. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 alikosa michezo ya mwisho ya msimu kutokana na tatizo hilo la kiafya.
Benchi la ufundi pamoja na madaktari wa timu hiyo wameamua kuchukua tahadhari kubwa katika mchakato wa kumrejesha nyota huyo ili kuhakikisha majeraha hayo hayajirudii tena. Kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi, Yamal amewekewa ratiba maalum ya mazoezi ya hatua kwa hatua kabla ya kurejea katika ushindani wa kawaida.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Taarifa zinaeleza kuwa Yamal anaendelea vizuri na maendeleo yake yanaonekana kuwa ya kuridhisha, huku akiongeza nguvu mwilini pamoja na kufanya mazoezi mepesi ya mpira. Hata hivyo, benchi la ufundi halitaki kuharakisha kurejea kwake mapema ili kulinda afya yake ya muda mrefu.
Kutokana na hali hiyo, kiungo huyo anatarajiwa kuukosa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Cape Verde. Uamuzi huo umefanywa ili kumpa muda zaidi wa kujiimarisha kabla ya kurejea uwanjani kwa asilimia mia moja.
Licha ya kukosekana kwake katika mchezo huo wa ufunguzi, mashabiki wana matumaini makubwa ya kumuona Yamal akirejea mapema katika michuano hiyo mikubwa duniani. Uwepo wake unatajwa kuwa muhimu kutokana na kiwango bora alichoonyesha kabla ya kuandamwa na majeraha.


