Mchezo wa El Clasico kati ya Real Madrid dhidi ya klabu ya Barcelona ambao ni mchezo wa fainali ya kombe la Spanish Cup utapigwa nchini Saudia Arabia leo kwa mara ya kwanza.
Real ambayo ilifanikiwa kuifunga klabu ya Valencia kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Spanish Cup ambalo limefanyika nchini Saudia Arabia mwaka watamenyana na klabu ya Fc Barcelona katika mchezo wa fainali.
Klabu ya Barcelona wao walifanikiwa kuwafunga mabingwa watetezi wa michuano hiyo katika mchezo wa nusu fainali kwa mikwaju ya penati na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali, Hivo kuwafanya kukutana na mahasimu wao klabu a soka ya Real Madrid.
Kyelekea mchezo huo kila timu inaonesha kuhitaji kubeba taji hilo ambalo litakua taji la pili kwa Los Blancos msimu huu, Lakini litakua la kwanza kwa klabu ya Fc Barcelona chini ya mwalimu Xavi Hernandez hivo unatarajiwa kua mchezo mkali na wakuvutia.
Vinara wa ligi kuu nchini Hispania kwasasa klabu ya Barcelona inaonekana imeanza kurejesha makali yake kitu ambacho kinafanya mchezo huo kivutio kikubwa, Kwani klabu ya Real Madrid wao wako kwenye ubora wao ambao wamekua nao tangu msimu uliomalizika.


