Aliyekuwa Golikipa wa klabu ya Bayern Munich Oliver Khan ameungana na klabu hiyo kwa kuingia kwenye bodi ya wakurugenzi wa klabu.
Legendari huyu ambaye aliteuliwa tokea mwezi Januari, alitarajiwa kuanza majukumu yake na bodi hiyo tarehe 1 Januari 2020.
Khan anatazamiwa kuchukua nafasi ya Karl-Heinz Rummenigge ambaye ni mwenyekiti wa klabu mwishoni mwa mwka 2021.
Staa huyu aliyetamba zamani ana umri wa miaka 50 na amecheza Jumla ya mechi 632 za ushindani katika miaka yake 14 na klabu ya Bayern Munich.
Khan aliamua kustaafu mwaka 2008, alianzisha taasisi ya Oliver Khan Foundation ili aweze kuirejeshea jamii kwa kuwasaidia wanajamii wenye changamoto za kijamii.
Rekodi zinamtaja staa huyu kuwa alianza kutambulika katika soka akiwa na umri wa miaka sita, akiwa anaichezea klabu ndogo ya nyumbani kwao na mwaka 1987 aliingia kucheza soka kwenye daraja la juu akiwa na klabu ya Karlsruher SC.
Bayern Munich walimsainisha mwaka 1994 kwa dau la dola milioni 2.5 ikiwa ni rekodi ya pekee kwa wakati huo kwa golikipa wa Kijerumani. Sasa anaingia kwenye majukumu ya uongozi wa juu wa klabu hiyo.
Gabriel
Miongon mwa makipa wagimu kufungika Oliver Khan