Hali inazidi kuwa mbaya kwa Chelsea baada ya serikali ya Uingereza kutaifisha mali za Roman Abramovich. Kampuni ya “Three” 3, yaomba kusitisha mkataba na The Blues.
Haya ni maamuzi ambayo 3 inayafikia wakiwa na lengo la chanya la kuendana na juhudi za serikali kuonesha msimamo wake dhidi ya vita ya Ukraine inayoendeshwa na Urusi. 3 ambayo ni kampuni ya mtandao wa simu, imeomba kusitisha mkataba wake na Chelsea kwa muda, mpaka pale itakapotolewa taarifa nyingine.
Mkataba uliokuepo kati ya kampuni hiyo na The Blues, ulikuwa ni kwenye eneo la matangazo ya kibiashara ambapo, nembo ya namba 3 ilikua inakaa upande wa mbele ya jezi za Chelsea pamoja na matangazo mengine ndani ya Stamford Bridge.

Pamoja na kusitisha mkataba na mahusiano yao na Chelsea, kampuni ya three imeeleza kuendelea kuwasaidia raia wa Ukraine wanaingia nchini Uingereza ambapo, kampuni hiyo itahakikisha inawapatia huduma za mawasiliano bila malipo ili waweze kuwasiliana na wapendwa wao.

Hali ya sintofahamu inaendelea kutanda ndani ya klabu ya Chelsea na mpaka sasa, haijulikani muenendo wa klabu hiyo utakuaje baada ya fursa za kiuchumi kufungwa na serikali kutokana na maamuzi ya kutaifisha mali za Abramovich nchini humo.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.



