Nyota wa klabu ya Real Madrid, Eden Hazard ameanza msimu kwa kusuasua akiwa na matatizo ya kifundo cha mguu ambayo yanamtesa wakati huu. Akiwa kama sehemu ya kikosi cha kwanza na akiwa katika mipango ya kocha wake amekumbana na matatizo ambayo yanampa wasiwasi sana kocha wake juu ya nini la kufanya katika nafasi yake.
Hazard alisainiwa akitokea Chelsea na amekuwa na mchango mkubwa kikosini hapo katika matokeo ambayo kikosi hicho kimekuwa kikiyapata japo majeraha ambayo amekuwa akikutana nayo yanampotezea nafasi ya ushindani zaidi nyota huyo. Katika hatua hiyo Madrid wanahitaji jitihada za haraka kwa nyota huyo.
Jambo kama hili linakuwa gumu kwa Madrid kumuachia Bale ambaye kuna wakati hucheza nafasi za aina hii mbali na kuwa ni mtu wa pembeni. Wanahitaji maangalizi ya haraka ya kitabibu kwa nyota huyo kutokana na kwamba tatizo la aina yake likizidi hupelekea usugu ambao kuutibu huchukua muda kiasi.
Akiwa katika majukumu ya timu ya taifa amekuwa msaada wa aina yake kikosini humo lakini pia hata Madrid wanaujua mchango wake akiwa uwanjani japo bado kuna changamoto ndogo ndogo za kuzoea ligi hiyo ambayo kwa sasa ipo katika ushindani mkubwa sana hasa kwa klabu kubwa kupambana sana wanapokutana na klabu zenye majina madogo.
Hazard anasubiri kuhudhuria vipimo vizito vitakavyofanyika juu yake ili kumsaidia mapema ili aweze kurejea uwanjani kupambana na kikosi hicho. Madrid ni klabu ya ndoto yake ndiyo maana anapambana kwa namna yoyote ili aweze kulipa fadhila ambazo kama klabu imeona uwezo wake wa kucheza katika klabu yao.
Katika mechi ambayo Hazard alitoka uwanjani wakati wa kipindi cha pili, Zidane amempa sifa za aina yake mlinda mlango wao wa zamani, Keylor Navas ambaye ameonesha umaridadi wa aina yake baada ya kuzuia michomo mikali ambayo kwa kawaida ilikuwa ni magoli ya wazi kabisa kwa Madrid.
Kwake nyota huyo wa zamani wa klabu hiyo ni mchezaji wake bora ndani ya mechi hiyo. Klabu hizo zilifanyiana mauziano mapema msimu huu juu ya walinda mlango hao wawili na Navas amebaki kuwa chaguo la kwanza kwa Tuchel kutokana na umaridadi wake na ukongwe wake alionao katika milingoti miwili iliyosimama.
Furahav
Pole sana.