Metacha Mnata Usije Sema Shetani Alikupitia

Katika kila baya alifanyalo mwana wa Adam basi kuna kisingizio cha shetani. Wengi wetu tumekua tukitamka kwa vinywa vyetu kwamba “SHETANI ALINIPITIA”. Akili imezoea sana majibu haya, ubongo umekwisha lewa kwa kauli za aina hii.

Inasemekana Shetani ndie adui mkubwa wa binadamu kuwahi kutokea hapa duniani, hakuna kiumbe chenye chuki na mwana wa adamu kama shetani. Miongoni mwa visa maarufu hapa duniani ni kisa cha shetani na sisi. Hapo mwanzo shetani alikua malaika, japo yeye aliumbwa kwa moto.

Baada ya Muumba wetu kuwaamuru malaika wote wamsujudie Adam ambaye aliumbwa kwa udongo, malaika wote walitii amri isipokua shetani. Shetani hakumtii muumba wetu. Na hapo ndipo shetani akalaaniwa na kupewa makazi ya motoni milele.

Bila hiyana shetani akamuomba muumba wetu asiende peke yake kwenye makazi ya moto, bali aende na baadhi ya wana wa Adam watakao muasi muumba wao. Tangu hapo shetani akatumia nguvu nyingi kumshawishi Adam na wana wake wamfuate kwenye makazi yake ya motoni.

Hiki ni kisa maarufu sana kwenye vitabu vingi vya dini. Nadhani sisi wana wa Adam tumesahau uadui wetu na shetani. Tunamuenzi sana kwa kutaja jina lake kwenye makosa ambayo tunayafanya kwa makusudi yetu.

Labda siku tuungane kwa pamoja kuomba msiba wa shetani utokee ili tusimuone tena na hata tusimuongelee. Nachukua nafasi hii kumuasa Metacha Mnata. Kipindi tunaomba dua ya kifo cha shetani basi na yeye asijisahau pale golini.

Goli alilofungwa na SEIF KARIE ni makosa yake, na sio mara ya kwanza kufungwa goli la aina ile. Kabla kauli za shetani alinipitia hazijatumika, basi tunakuomba metacha urekebishe hapo padogo kwani wewe ni tegemeo la taifa siku chache zijazo.

Seif Karie

Ukiendelea kutumia usemi wa shetani basi kumbuka tu kwamba kule benchi yupo Ramadhani Kabwili, yupo pia Farouk Shikalo. Wote hawa ni wazuri mno, na si kwamba unawazidi kila kitu, bali kuna padogo ulipowazidi. Kwa kutambua hilo basi nadhani hutojisahau tena.

Farouk Shikalo na Ramadhani Kabwili

Nadhani mmewahi kuyaona masaibu ya Kepa Arrizabalaga wa Chelsea, golikipa aliyeimbwa sana na wana London. Leo yuko wapi.. enyi mlio karibu na Metacha.. ongeeni naye, muonesheni clip za KEPA, kisha mwacheni.

 

Kepa Arrizabalaga

VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

9 Komentara

    Ama kweli dunia imeisha tunafanya wenyewe makosa halafu tunamsingizia shetani inabidi wanaa adam tubadilike mara moja

    Jibu

    Duu ila sio poa shetani amekula sababu

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    🤣🤣🤣

    Jibu

    Metacha ni noma huyu kipa

    Jibu

    Metacha noma

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Hakuna mtu hapitiwi na shetani

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.