Klabu ya Ac Milan wamekubaliana na mlinzi wa klabu ya LOSC Lille Sven Botman kuhusu uhamisho wake ambapo wiki iliyopita walikuwa na mazungumzo na klabu yake kuhusu uhamisho wa wachezaji wawili.
Ac Milam awali walikuwa na mazungumzo na klabu ya Lille kuhusu uhamisho wa wachezaji wawili, ambao ni mlinzi wa kati Sven Botman na kiungo Renato Sanches na sasa wanaenda kamilisha usajiri wa mmoja wapo.
Ac Milan bado ipo kwenye mazungumzo na Sanches ili kuweza kukamilisha usajiri wake, Lille ikiwa tayari ishakubaliana na Milan, makubaliano binafsi kati Milan na mchezaji ndio yanayokwamisha, usajiri wa wachezaji wote wawili utagharimu kiasi cha £40milioni, huku Botman akiwa na thamani ya £25milion, Sanches £15milioni.
Ac Milan kwa sasa wanafurahia msimu bora chini ya kocha Stefano Pioli, huku akiwa kileleni mwa ligi Serie A, huku kukiwa na michezo saba tu iliyobakia ili ligi hiyo imalizike.
Sven Botman muda wowote kuanzia sasa anaweza kumwaga wino kwenye klabu hiyo, huku akitarajiwa kutengeneza safu ya ulinzi na muingereza Fikayo Tomori msimu ujao.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.