Mabingwa wa nchini Italia Serie A wamekamilisha usajiri wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji Divock Origi kutoka klabu ya Liverpool kwa uhamisho huru.

Divock Origi ameondoka nchini Uingereza baada ya kuishi kwa muda wa miaka nane na akiwa kwenye viunga vya dimba la Anfield, huku kwenye msimu wa 2014-15 alipelekwa kwa mkopo nchini Ufaransa kwenye klabu ya Lille, pia msimu wa 2017-18 alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Wolfsburg.

 Divock Origi

Origi kwa kipindi alichokuwepo katika klabu ya Liverpool atakumbukwa kama mshmbuliaji bora akitokea benchi, huku akiacha kumbukumbu ya kufunga goli la ushindi dhidi ya klabu ya Everton kwenye dakika 95 mwaka 2018, pia mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona ambapo alifunga mara mbili.

Divock Origi amefanikiwa kufunga magoli 11 akitokea benchi, huku akiwa mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi zaidi akitokea benchi kwenye klabu ya Liverpool.

Origi ameichezea klabu ya Liverpool michezo 175, huku akifanikiwa kufunga magoli 41 kwenye mashindano yote.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa