Ac Milan Wajipanga Kumzodoa Donnarumma

Mashabiki wa Ac Milan wanajipanga kumzodoa aliyekua golikipa wa klabu hiyo Gigi Donnarumma ambaye anakipiga ndani ya klabu ya PSG kwasasa kwa kumtupia pesa uwanjani.

Mashabiki wa klabu ya Ac Milan wanamuona Donnarumma kama msaliti na aliondoka ndani ya timu hiyo na kujiunga na klabu ya PSG kwasababu ya pesa na ndio jambo ambalo limefanya mashabiki wa klabu hiyo kupanga kumrushia pesa mchezaji huyo.donnarummaGolikipa Donnarumma atarejea katika dimba la Sansiro kwa mara ya kwanza tangu aondoke ndani ya klabu hiyo mwaka 2021 na kujiunga na klabu ya PSG katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu yake ya zamani.donnarummaMashabiki wa Ac Milan wameshawahi kufanya kitendo cha kumtupia pesa Donnarumma wakimuona kama msaliti wakati akihusishwa kuondoka klabuni hapo miaka kadhaa nyuma, Lakini leo wanapanga kurudia kitendo walichowahi kukifanya hapo nyuma kwa golikipa wao huyo wa zamani.

Acha ujumbe