Adam lallana mchezaji wa klabu ya Brighton and Hove Albion inaelezwa atakua kocha wa muda ndani ya klabu hiyo mpaka atakapopatikana mwalimu mpya.

Brighton kwasasa hawana kocha mkuu baada ya kocha wao mkuu Graham Potter kuelekea kwa matajiri wa London siku ya alhamisi na kusaini kandarasi kuwatumumikia Chelsea kwa miaka mitano na kuwaacha klabu yake hiyo ya zamani bila kocha.

adam lallanaKutokana na hali hiyo viongozi wa Brighton inaelezwa wanafikiria kumpatia timu Lallana kama kocha mchezaji mpaka pale timu hiyo itakapopata mwalimu wa kudumu.

Adam Lallana mchezaji wa zamani wa vilabu vya Southampton na Liverpool atakua sio mchezaji wa kwanza kua kocha mchezaji kwenye timu kwani kuna wachezaji kama Ryan Giggs ambae alikua kocha mchezaji ndani ya Manchester United msimu wa 2013/14 baada ya kocha kuondolewa pia Ruud Gulit ambapo alisimama kama kocha mchezaji ndani ya Chelsea mwaka 1996 mpaka mwaka 1998 vilelvile Muitaliano Gianluca Vialli ambae alikua kocha mchezaji mwaka 1998 mpaka mwaka 2000.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa