Kocha Mkuu wa Morocco Herve Renard snsschis ngazi baada ya Morocco kushindwa kutoboa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa -AFCON. Morocco walikuwa wanatarajiwa kuwa moja ya timu ambayo ingesumbua sana mapema kabla ya kuanza kwa michuano hii.
Hata hivyo, hawakuwa na bahati baada ya kutolewa kwenye hatua ya mtoano wa timu 16 walipokubali kichapo kutoka kwa Benin kwa mikwaju ya penati.
Kocha huyu alifanikiwa kushinda AFCON mwaka 2012 akiwa na Zambia, pia mwaka 2015 akiwa na Ivory Coast. Amekuwa meneja wa Benin toks mwaka 2016. Renard, anafikiri kuwa huu ni wakati wake muafaka wa kuachana na majukumu aliyokuwa nayo kama meneja wa Morocco.
“Ni wakati wa kuufunga ukurasa mrefu na mzuri wa maisha yangu…. ni uamuzi ambao nimeufanya baada ya kufanya tafakari kwa umakini. Hivyo ni uamuzi ambao hauwezi kutenguliwa.”
Hata hivyo, uamzi huu unaonekana kuwa tayari ulikuwa umefikiriwa kabla ya michuano ya AFCON 2019.
Renard aliifanikisha Morocco kupanda kwenye viwango vya FIFA kutoka nafasi ya 81 hadi kufikia nafasi ya 47. Aliwaongoza katika michuano ya Kombe la Dunia 2015, na pia kwenye michuano ya AFCON.
Zeiyana
Asante kwa makala