Mshambuliaji wa timu ya Barcelona Sergio Agüero alikimbizwa hospitali baada ya kusumbuliwa na tatizo la maumivu ya kifua na kulalalmika kuwa anajisika kizunguzungu kwenye mchezo ligi kuu ya Hispania La Liga dhidi ya Alaves jana jumamosi na mchezo huo kuisha kwa sare ya 1-1.
Wakati mchezo ukiwa unaendelea kwenye kipindi cha kwanza Aguero alionesha ishara ya kuomba kutolewa, na alitoka huku nafasi yake ikichukuliwa na Philippe Coutinho.

“Nilimbiwa alikuwa anajisikia kizunguzungu, ninachojua alichukuliwa na kupelekwa hospitali na siwezi sema zaidi mapaka nijue.” alisema kocha wa muda wa barcelona Sergi Barjuan
Aguero alionekana akiwa amelala chini hiku akiwa amejishika kifua kabla madaktari kuwahi kwenda kumsaidia na kisha kusimama na kutoka nje ya uwanja akitembea pasipo usaidizi, Depay alifunga goli la ufunguzi kwa Barcelona dakika 49 kipindi cha pili, kabla ya Luis Rioja kusawazisha dakika tatu mbele.

Mchezo wa kwanza kwa Sergi Barjuan akiwa kocha wa muda ametoa sare ya 1-1, Barcelona ipo nafasi ya tisa ikiwa nyuma ya apointi 8 dhidi ya kinara wa ligi Real Madrid, Real Madrid imefanikwa kuifungu Elche goli 2-1, Vinícius Júnior akifunga magoli yote mawili na goli pekee la Elche likifungwa na P. Milla.
JIUNGE KWENYE SHINDANO LETU LA EXPANSE NA USHINDE!
Achana na ndoto za usingizini za kuokota burungutu la pesa, amkia upande wa ushindi halisi kutoka Meridanbet kwenye shindano la Expanse linalojumuisha michezo pendwa ya sloti za mtandaoni iliyopo kwenye promosheni ya Expanse kutoka Meridianbet.


