Nguli wa Manchester City, Sergio Agüero, amethibitisha kuwa atafanyiwa upasuaji baada ya kupata jeraha kubwa wakati wa mechi ya wachezaji wakongwe nchini Argentina. Tukio hilo lilitokea katika pambano la +35 kati ya Independiente na River Plate, ambapo alitolewa uwanjani akiwa na maumivu makali.

Kilichotarajiwa kuwa sherehe kwa mashabiki wa Independiente kiligeuka huzuni, baada ya mshambuliaji huyo wa zamani kuanguka bila kuguswa na mchezaji yeyote. Mechi hiyo iliyochezwa Wilde Stadium ilimalizika kwa ushindi wa 2-0 kwa Independiente, ila macho yalikuwa kwa Agüero aliyebebwa nje ya uwanja na kupelekwa kufanyiwa vipimo.
Kupitia ujumbe wake, Agüero alithibitisha kuwa amechanika Achilles, jeraha ambalo linahitaji upasuaji wa haraka. Ameweka wazi kuwa hakuna njia nyingine zaidi ya kufanyiwa operesheni, huku akiwashukuru wachezaji wenzake na wapinzani kwa msaada wao wa haraka wakati wa tukio hilo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Jeraha hili linakuja kama pigo kwa Agüero ambaye alikuwa ameanza kurejea taratibu kucheza katika ligi za wakongwe na kuonyesha dalili za ubora kwa kufunga mabao. Alikuwa ameonyesha nia ya kuendelea kucheza mechi zaidi na kuisaidia timu yake ya zamani, lakini sasa mipango hiyo imelazimika kusitishwa.

Hii ni changamoto nyingine kubwa kwake tangu alipostaafu soka la ushindani mwaka 2021 kutokana na matatizo ya moyo alipokuwa FC Barcelona. Sasa lengo kuu ni kufanikisha upasuaji na kuanza safari ya kupona, huku mashabiki duniani wakimtumia salamu za pole na kumuombea apone haraka.



