Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri yamtambulisha kocha wake mpya Marcel Koller ambaye ataenda kukinoa kikosi hicho kwa msimu huu ambao umeanza. Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya Taifa wa Austria.

 

Al Ahly Yamtambulisha Kocha Mpya

 

Ahly imemtangaza kocha huyo ambaye ataenda kurithi nafasi ya kocha Ricardo Soares ambaye ametimuliwa wiki iliyopita baada ya kushindwa kutetea ubingwa wao ambao wameukosa mara mbili mfululizo.

Kocha Ricardo nae alikuja mara baada ya kutimuliwa Pitso Mosimane ambae alidumu na miamba hiyo ya Misri muda mrefu na timu ambayo imechukua kombe la klabu bingwa Africa mara nyingi. Mosimane amepata mafanikio mengi na Ahly kwani amebeba makombe mengi akiwa na timu hiyo ikiwemo kombe la ligi, klabu bingwa na mengine mengi hapo Misri.

 

Al Ahly Yamtambulisha Kocha Mpya

Kwa upande wa klabu hiyo kufukuza makocha kunatona na presha kubwa wanayopata kutoka kwa wapinzani wao na mahasimu wakubwa Zamaleck ambao wamekuwa na ubora misimu miwili mfululizo na kuchukua kombe hilo mara mbili kitu hicho kinafanya makocha kutodumu kwani usipofikia malengo lazima ufukuzwe.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa