Ahmed Ally Meneja wa Idara Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa ufungaji wa mabao kwa mshambuliaji wao mpya Steven Mukwala sio wa kawaida kutokana na kufanya maamuzi magumu kwenye nyakati ngumu.
Ikumbukwe kwamba Mukwala ni chaguo la pili la Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids chaguo la kwanza ni Leonel Ateba na wote wawili wametupia mabao mawili ndani ya ligi.
Bao la pili Mukwala alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa dakika ya 90 akitumia pigo la kona ya Awesu Awesu walipokomba pointi tatu mazima kwenye mchezo huo Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Ahmed Ally amesema mahesabu makubwa yanatumika na mshambuliaji huyo kufanya kazi ndani ya uwanja kwenye ufungaji jambo ambalo linawapa nguvu kwenye kusaka ushindi kwenye mechi ambazo wanacheza uwanjani.
“Unaona namna ambavyo Mukwala anafunga mabao yake ni magumu na sio ya kawaida kutokana na wachezaji kufanya maamuzi magumu kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo ni muda wetu kuendelea kuwapa burudani mashabiki.
“Bado kazi inaendelea kuna mechi ambazo zipo na tunahitaji kufanya kazi kubwa kwenye mechi zinazokuja hii inawezekana kutokana na uimara wa wachezaji waliopo hivyo muda upo mashabiki tuzidi kuwa pamoja.”