Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally, amesema kikosi hicho bado kina nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye michezo ya awali.
Ahmed ameeleza kuwa Simba imebakiwa na fursa moja muhimu ya dhahabu, hususan katika mchezo wa marudiano wa nyumbani utakaochezwa Februari 01, akisisitiza kuwa matokeo ya mechi hiyo yatakuwa na mchango mkubwa katika mwelekeo wa timu hiyo kwenye kundi.
Simba inatarajia kushuka dimbani Februari Mosi mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ikisaka ushindi dhidi ya Esperance Sportive de Tunis katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki.
Mbali na mchezo huo wa nyumbani, Simba pia itakuwa na kibarua kingine kigumu cha kusaka alama sita dhidi ya Petro de Luanda ugenini kabla ya kurejea nyumbani kuikabili Stade Malien, michezo ambayo imeelezwa kuwa ya msingi katika kufufua matumaini ya timu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ahmed amesisitiza kuwa michezo hiyo mitatu iliyobaki ni muhimu sana katika safari ya Simba ya kupigania kufuzu kwenda hatua ya robo fainali, akibainisha kuwa bado hakuna sababu ya kukata tamaa kwa kuwa kila kitu kiko wazi.
Ameongeza kuwa namna ambavyo Simba imekuwa ikicheza pamoja na juhudi kubwa zilizooneshwa na wachezaji katika michezo iliyopita, kunatoa matumaini makubwa ya kupata matokeo chanya kwenye michezo ya mwisho ya kundi.



