AHMED ALLY MATUMAINI KIBAO KIMATAIFA

Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wa klabu hiyo Ahmed Ally umebainisha kuwa utaonyesha ubaya ubwela kwenye mchezo wao wa kimataifa dhidi ya SC Sfaxine kwa lengo la kufufua matumaini kutinga hatua ya robo fainali.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 15 ikiwa ni mchezo wa tatu kwa Simba katika anga la kimataifa ikiwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya CS Constantine licha ya kuanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 24 kupitia kwa Mohamed Hussen.ahmed allyAhmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji kupata ushindi.

“Ni ubaya ubwela kwenye mchezo wetu dhidi ya SC Sfaxine hakuna namna tumepoteza mchezo uliopita licha ya kwamba tulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda ila matokeo yamepita na sasa ni hesabu kuelekea mchezo ujao.

“Tuna timu bora hivyo ni muda wa kila Mwanasimba kuinuka na kununua tiketi halafu asisahau aje uwanjani kwa kuwa huu ni mchezo muhimu na mgumu licha ya kwamba tutakuwa nyumbani kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo na mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani huku wakishangilia mwanzo mwisho Uwanja wa Mkapa.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.