Ndani ya Ligi Kuu Bara Tanzania, kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 22 kati ya 25 ambazo wamecheza na kukusanya pointi 61.
Ikiwa imefungwa jumla ya mabao 10, Manula ameokota nyavuni jumla ya mabao 9 katika mechi 8 ambazo alifungwa huku akikusanya jumla ya clean sheet 14.
Ni mechi 22 ambazo amekaa langoni huku mechi mbili pekee akifanyiwa mabadiliko ilikuwa mbele ya KMC alipotumia dakika 45 na mbele ya JKT Tanzania alitumia dakika 67.
Jumla ametumia dakika 1912 na ana wastani wa kuokota bao moja nyavuni kila baada ya dakika 212.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Magdalena
Manula goalkeeper makini