Klabu ya Ajax Amsterdam wao wameendelea kukubali vichapo kunako ligi kuu ya Uholanzi baada ya leo kupoteza mchezo wa derby mbele ya mahasimu wao klabu ya Psv Eindhoven.
Psv Eindhoven wamefanikiwa kuichabanga klabu ya Ajax kwa mabao matano kwa mawili katika mchezo huo wa derby na kuendelea kuifanya klabu hiyo kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ya Uholanzi.
Mabingwa hao wa ligi kuu ya Uholanzi wamekua kwenye kipindi kigumu sana hivi karibuni kwani matokeo ya klabu hiyo yamekua sio ya kuridhisha hata kidogo jambo lililopelekea kumfukuza kocha wao wiki hii.
Klabu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu tangu mwezi wa nane mwaka, Huku michezo mingi ikiwa imepoteza jambo ambalo linaiendelea kuifanya klabu hiyo kudidimia zaidi.
Msimamo wa ligi kuu ya Uholanzi maarufu kama Eredivise mpaka sasa anaeshika mkia ni klabu ya Ajax wakiwa katika nafasi ya 18 na alama zao tano, Hii ikiwa ni jambo la kushagaza kabisa katika historia ya klabu hiyo.