Ajax wamejaribu kufanya ambacho wengi hawakukitarajia, kumfuata kocha wa Liverpool, Arne Slot, katika harakati za kutafuta kocha mpya wa kudumu. Hata hivyo, jitihada hizo zimegonga mwamba mapema, baada ya Mholanzi huyo kuonyesha hana mpango wa kuondoka Anfield licha ya kuwa na msimu mgumu.

Chini ya mkurugenzi wa ufundi Jordi Cruijff, Ajax wanapitia kipindi cha kujipanga upya wakitafuta kiongozi sahihi wa kuirejesha timu kwenye ubora wake wa zamani. Ingawa Michel wa Girona anaonekana kuwa chaguo la mbele, jina la Slot liliongezwa kwenye orodha ya makocha wachache wanaoaminika kuwa na uwezo wa kuibeba Ajax, sambamba na Peter Bosz ambaye tayari ameongeza mkataba wake PSV.
Ripoti zinaeleza kuwa Ajax waliulizia uwezekano wa kumpata Slot, lakini majibu hayakuwa ya kutia moyo. Inasemekana wazi kuwa kocha huyo yuko imara Liverpool na hana nia ya kurejea Uholanzi kwa sasa. Hii inaonyesha kuwa bado ana imani na mradi wake ndani ya Ligi Kuu England.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Umaarufu wa Slot unatokana na mafanikio yake makubwa akiwa Feyenoord, ambapo aliwahi kutwaa ubingwa wa Eredivisie na Kombe la KNVB, pamoja na kufika fainali ya Conference League. Licha ya kushuka kwa kiwango kidogo na Liverpool msimu huu, bado ana mkataba hadi 2027 na anaonekana kujenga kitu cha muda mrefu.

Kwa sasa, Ajax wanalazimika kuangalia njia nyingine huku wakijiandaa na mabadiliko makubwa ya kiutawala. Wakati huo huo, Slot ana kazi nzito mbele yake kuhakikisha Liverpool wanamaliza msimu vizuri na kupata nafasi ya kushiriki Champions League. Hii ni vita mbili tofauti, Ajax wakitafuta mkombozi, na Slot akilinda heshima ya Liverpool.



