Imeripotiwa kuwa wababe wa Cairo, Al Ahly wako kwenye harakati za kukamilisha uhamisho mkubwa kwa mshambuliaji wa Raja Club Athletic ya Morocco, Soufiane Rahimi katika dirisha lijalo la uhamisho wa kiangazi.
Rahimi hatokuwa usajili wa kwanza kutoka Raja Casablanca kwenda Al Ahly mwaka huu, kwani Mashetani Wekundu wamemsajili Beki Badr Benoun msimu uliopita wa kiangazi kutoka kwa wababe hao wa Morocco pia kwa pesa nyingi.
Mchezaji huyo wa miaka 24 amecheza mechi 26 kwenye mashindano yote ambapo alifunga mabao 10 na kutoa assists nane.
Kulingana na chapisho la MoroccoAlmountakhab, Al Ahly wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsainisha Rahimi kutoka Raja msimu wa joto, wamewasilisha ofa ya kwanza ya $5m (Tshs 11.5b) ili kupata huduma za Rahimi, ambaye alianza kuitumikia Morocco mnamo Machi 26 dhidi ya Mauritania.
Pitso Mosimane hakuwa na ubora mzuri kutoka kwa washambuliaji wa Al Ahly msimu huu iwe kwenye Ligi Kuu ya Misri au Ligi ya Mabingwa Mbali na Mohamed Sherif, washambuliaji wengine watatu kwenye orodha ya Al Ahly, Marwan Mohsen, Salah Mohsen na Walter Bwalya, wamechangia jumla ya mabao matatu kwa timu msimu huu.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Asanteni kwa taarifa
Asante kwa makala
Wakimpata watakuwa wamelamba dume
Nice update
Wafanye mpango wampate
Itakua poa.
Wajitahidi wampate
Safiiii
Wakimpata itakua pw sana
Mchezaji mahili
Safi
Wajikaze wafanye juu chini wampate tu
Waweke dau la maana
Itakuwa pos
Itakuwa poa
Safi
Kilaraheri
Itakuwa poa
Wakimakinika wanampata
Nice