Mwanariadha kutoka Nairobi, Kenya amekutana na rungu kali la bodi inayosimamia michezo yao kwa kufanya kosa la kinidhamu. Mkenya huyo amesimamishwa kushiriki michezo kwa kupewa adhabu na Atheltics Integrity Unit (AIU) baada ya kushindwa kueleza ni wapi alikuwa wakati akitafutwa, tayari anaitumikia adhabu hiyo.
Hii inakuja ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu bingwa wa 2017 London Marathon, Daniel Wanjiru kupigwa rungu kama hilo na bodi hiyo hiyo ya AIU.
Korio, ambaye ni bingwa wa 2017 Bengaluru 10 kilometa, pia, alikuwa ni sehemu ya waliochuana vikali na Eliud Kipchoge katika shindano la Ineos 1:59 nchini Vienna mwaka jana na mbio zake za mwisho kushiriki ni zile za umbali wa 10 kilometa zilizofanyika Valencia.
Mwanariadha huyu aliwakilisha taifa lake la Kenya kwenye 2019 World Athletics Championship ambapo alikuwa ni mshindi wa nafasi ya 11 kwenye mbio za umbali wa mita 10,000. Kwenye ubingwa wa kitaifa hivi karibuni alishika namba nne kiujumla.
Kwa adhabu hii sasa Korio anakuwa ni Mkenya wa sita kukutana na rungu la AIU baada ya Wanjiru, mwanamarathoni wa zamani aliyevunja rekodi ya kidunia Wilson Kipsang, Alfred Kipketer, Kenneth Kiprop na Mikel Kiprotich Mutai ambapo huyo wa mwisho alipizuiwa kwa kuwa na Madawa Yasiyoruhusiwa Michezoni (Norandrosterone).
SADICK
Duh! Pole yake
Gabriel
Sio kosa kubwa la kumpatia adhabu hiyo ikichukulia huyu n mwanariadhara bora dunian kwa kosa dogo kama hilo
Neema juma
Kajiharibia sifa. Pole yake
povel
pole sana wa kenya ila udanganganyifu kwenye michezo cyo vzr
Zeiyana iddi
Pole kijana..!azabu itaisha mambo mengine yataendelea..!
Neema hassan
Lazma Sheria zifuatwe ili iwe funzo kwa wengine…
hamidu
sheria lazima ifatwe..baadhi ya wana-riadha wababaifu
Elika
Pole yake.atajifunza kutokana na makosa
Mwajuma
Mnatujuza mambo mengi ambayo hata atuyajue asanten kwa hilo
mwakalosi
Inaonekana wanatumia mazoea sana kuliko nidhamu ys mchezo
Asia Abdy
Hatua za kinidham lazma zichukuliwe
Neema hassan
Lazma Sheria zifuatwe ili iwe funzo kwa wengine…
Adelta
Udanyanyifu sio mzuri pole yake
Winfrida
Natumaini atajifunza atorudia tena
David Pere
Jamaa kajiharibia Sana kutumia madawa yaliyokatazwa michezoni
Rehema Dickson
Iyo safi sana na iwe funzo kwa wote wenye tabia kama zake
Agness
Kajiharibia kazi na hiyo iwe fundisho kwa wengine
Khadija
lazima apeww adhabu
Furahav
Wamemuonea tu.
felister
safi sn cku nyngn atajifunza
lombo
duuuh
Mariam mtandama
Duuuh
Evaluziga
Pole yake amejifunnza kutokana na makosa