ALI KAMWE AKUBALI KUCHUTAMA

Ali Kamwe, Meneje awa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga amesema kuwa hawakuwa na mchezo mzuri tangu dakika ya kwanza mbele ya Tabora United hivyo wameyapokea matokeo kinyonge wanaamini watarejea kwenye ubora.

ALI KAMWE AKUBALI KUCHUTAMA

 

Ikumbukwe kwamba Novemba 7 2024, Yanga ilipoteza mchezo wake wa pili kwenye ligi baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Yanga 1-3 Tabora United.

Mchezo wa kwanza kupoteza msimu wa 2024/25 ilikuwa ni Novemba 2 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 0-1 Azam FC hivyo katika mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180, Yanga imepoteza pointi sita ilizokuwa inasaka ndani ya uwanja.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Ali Kamwe amesema kuwa wanatambua mashabiki, wachezaji na viongozi hawafurahii matokeo hayo kwa kuwa hayakuwa kwenye mpango hivyo wanaamini yatapita na Maisha yataendelea.

ALI KAMWE AKUBALI KUCHUTAMA

“Hiki ni kipindi cha mpito kwa kweli hakuna ambaye alitegemea matokeo ya aina haya, hatukuwa na mchezo mzuri tangu mwanzo wa mchezo wetu dhidi ya Tabora United kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya 90.

“Kilichotokea ni mpira na tunaamini kwamba benchi la ufundi limeona na makosa yatakwenda kufanyiwa kazi tunaamini kwamba tutarejea tukiwa imara zaidi kwenye mechi zijazo hilo linawezekana.” Alisema Ali Kamwe.

Kwenye msimamo, Yanga ni namba mbili ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 10 vinara ni Simba wana pointi 25 nao pia wamecheza mechi 10.

Acha ujumbe