Alisson Aibua Maswali Liverpool, Juventus Yaanza Kumfukuzia

Mustakabali wa Alisson Becker huko Liverpool umeanza kuzungukwa na maswali, huku Juventus ikiripotiwa kurejea kwenye rada ya kumsajili kipa huyo Mbrazil wakati Reds wakitafakari mpango wao wa kizazi kijacho kwenye lango.

Alisson Aibua Maswali Liverpool, Juventus Yaanza Kumfukuzia

Alisson, mwenye miaka 33, bado ni chaguo la kwanza Anfield na ameendelea kuonyesha ubora wake kwa kufanya saves muhimu. Hata hivyo, uwepo wa Giorgi Mamardashvili kama mrithi anayesubiri pamoja na kutokuwepo kwa mazungumzo mapya ya mkataba kumeongeza sintofahamu kuhusu maisha yake ya baadaye Liverpool.

Kwa mujibu wa Football Italia, Juventus inaweza kufufua nia yake ya kumsajili Alisson baada ya kushindwa kumpata katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Liverpool bado haijaanza rasmi mazungumzo ya mkataba mpya na Alisson, licha ya klabu hiyo kutumia kipengele mapema mwaka huu kilichoongeza muda wa mkataba wake hadi mwisho wa msimu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Alisson Aibua Maswali Liverpool, Juventus Yaanza Kumfukuzia

Kwa upande wa Juventus, hitaji la kipa limekuwa kubwa zaidi baada ya Kamil Grabara kufanyiwa upasuaji wa goti na kutarajiwa kuwa nje kwa miezi sita hadi saba. Klabu hiyo imeleta pia kipa mkongwe Neto kama suluhisho la muda.

Hata hivyo, Liverpool hawana kipa anayeshuka kiwango. Alisson ameanza kila mchezo wa Ligi Kuu England msimu huu na alionyesha tena ubora wake katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Bournemouth, ambapo save yake ya haraka dhidi ya Evanilson ilimuweka kwenye orodha ya waliowania tuzo ya Premier League Save of the Month.

Kipa huyo pia amefikisha clean sheets 138 katika mechi 336 alizoichezea Liverpool, rekodi inayomuweka nafasi ya nne kwenye orodha ya makipa wenye clean sheets nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Alisson Aibua Maswali Liverpool, Juventus Yaanza Kumfukuzia

Kwa sasa, Alisson bado ni nguzo muhimu ya Liverpool, lakini ukaribu wa Mamardashvili na ukimya kuhusu mkataba mpya vinaweza kufanya dirisha la 2027 kuwa kipindi cha maamuzi makubwa. Juventus, kwa upande wake, inaonekana bado haijaufunga mlango wa kumfuatilia Mbrazil huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.