Golikipa wa Liverpool, Allison ameomboleza kifo cha baba yake mpendwa na kuwashukuru mashabiki kwa sapoti yao katika kipindi hiki kigumu.

Baba wa golikipa huyu, Jose Agostinho Becker aliripotiwa kuwa amefariki baada ya kuzama majini akiwa anaogelea karibu ya nyumba yake ya likizo huko Brazil. Baada ya taarifa kutoonekana kwake alitafutwa na hatimaye mwili wake uliripotiwa.

Kilikuwa ni kipindi kigumu kwa nyota huyu kwa mujibu wa maelezo yake, lakini yeye na familia yake wanatoa shukrani zao kwa mashabiki, na watu wa karibu waliokuwa nao pamoja na kuwapa sapoti ya hali na mali.

Allison

“Ningependa kumshukuru kila mmoja kwa jumbe na heshima kwa baba yangu kipenzi. Famila yetu inahisi kupendwa na kila mtu! Mungu abariki maisha ya kila mmoja.” Unasomeka ujumbe wa Allison aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Liverpool bado wanaendelea kupambana kurejea kwenye fomu nzuri baada ya kuwa na sehemu kubwa ya msimu isiyoridhisha.


 

TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

Allison, Allison Amuomboleza Baba Yake, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa