Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Nchini Mohamed Mchengerwa amemteua Ally Mayay Tembele kuwa Kaimu Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya michezo Nchini akichukua nafasi ya Yusufu Omary Singo.

 

Ally Mayay (47) Ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo.

Katika kuimarisha utendaji kwenye sekta ya maendeleo ya michezo nchini leo Waziri  Mchengerwa amemteua Ally huku lengo likiwa ni kuboresha michezo nchini ikiwemo maendeleo ya timu za Taifa kwa ngazi zote.

Kabla  ya uteuzi huo  alikuwa ni  mchambuzi wa Azam Tv na afisa mwandamizi katika mamlaka ya viwanja vya ndege nchini. Aidha uteuzi huo unaanza kufanya kazi kutokana na maelekezo ya Wizara husika.

Ally Mayay (47) Ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa