Miguel Almiron hana kinyongo na Jack Grealish kutokana na kile ambacho alichokiongea mchezaji huyo na angepeana nae mkono wake, licha ya mbwembwe za mchezaji huyo wa Manchester City.

Grealish alipendekeza mchezaji mwenzake Riyad Mahrez alicheza kama Almiron baada ya kubadilishwa katika ushindi wa City dhidi ya Aston Villa na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza siku ya mwisho ya msimu uliopita.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza tangu wakati huo amekiri kuwa anajutia maoni hayo aliyoyatoa katika klipu ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akirejelea uchezaji wa Almiron ambao hapo awali aliichezea Newcastle.
Kiwango cha Almiron tangu wakati huo kimepanda, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Paraguay akifunga mabao saba katika mechi nane akiwa na Newcastle kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia na anasisitiza kuwa hana matatizo na Grealish.

Almiron aliliambia gazeti la The Daily Mail: “Sikuwa makini sana, nilikuwa likizo na familia yangu. Na sikuwa na ishara ya simu ya mkononi! Kwa hivyo hapana, sikutazama video.”
Almiron alisema kuwa hapendezwi na hilo, Jack ni mchezaji mzuri na nitamtakia kila la heri. Yuko Manchezster City kwasababu ni mzuri na anaepuka kujilinganisha nae. Hivyo yeye anazingatia kile anachokifanya.
Almiron anaamini msamaha wa Grealish unaonyesha tabia ya mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27.

Aliongeza kwa kusema kuwa aliona mahojiano na kusikia kwamba alizungumza vyema kumhusu yeye na hawajawahi kuwa na chochote dhidi ya Jack na amekuwa akisisitiza kwamba anadhani yeye ni mchezaji mzuri na mtu mzuri.
“Hakujawahi kuwa na suala lolote kwangu. Yalikuwa mahojiano mazuri na ukweli kwamba alizungumza jinsi alivyofanya unaimarisha aina ya mtu alivyo. Ningempa mkono, hakuna shida.”

Mchezaji huyo atarejea kwenye mechi ya Primia Ligi akiwa na Newcastle huko Leicester siku ya Jumatatu.


