Amad Diallo Kutimkia Sunderland.

Amad Diallo kinda huyu wa Manchester United raia wa Ivory Coast anakaribia kujiunga na klabu ya Sunderland inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Uingereza.

Winga huyo ambae amekua akitolewa kwa mkopo hii itakua mara ya pili kwa kinda huyo kutolewa kwa mkopo kwani msimu uliomalizika alitolewa kwa mkopo kwa klabu  ya Rangers ya uskochi.

amad diallo

Amad aliejiunga klabuni hapo akitokea nchini Italia katika klabu ya Atalanta ambapo alikua akifanya vizuri na Man United kuvutiwa nae na kumsajili kijana huyo, Lakini kutokana na ufinyu wa nafasi kikosini hapo United wameona njia ya kumpatia nafasi ya kucheza kijana huyo kumtoa kwa mkopo vilabu vingine ili apate nafasi ya kucheza na kupata uzoefu ambao utakuja kuisadia Manchester United hapo baadae.

Kinda huyo atajiunga na Sunderland kwa mkopo wa msimu mzima wa 2022/23.

Acha ujumbe