Kuelekea usajili wa dirisha dogo mwezi Januari, Man United kuendelea walipoishia kwenye usajili wa majira ya kiangazi. Amad Diallo mbioni kukamilisha usajili wa kujiunga na United.
Man United walimsajili Amad Diallo mwishoni mwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi lakini kutokana na muda kutokuwa rafiki, usajili wa kinda huyu raia wa Ivory Coast haukukamilika kwa wakati na hivyo ilibidi kusubiri mpaka dirisha dogo la usajili.
Siku hazigandi, Januari 2021 ipo kwenye kona. Baada ya United kukamilisha taratibu zingine za usajili wa Diallo ikiwa ni pamoja na kumtangaza kama mchezaji wa klabu hiyo kupitia ukurasa rasmi wa timu hiyo, imeripotiwa kuwa Diallo ameshakabidhiwa hati ya uraia ya Italia na sasa ni suala la muda tu na punde atatua United.

Kutokana na utaratibu mpya ambao nchi ya Uingereza umeueka na utaanza kufanya kazi kuanzia Januari 1, kulikuwa na mashaka kama usajili wa Amad Diallo utakamilika kabla ya makubaliano ya Governing Body Endorsement kuanza kutumika.
The Governing Body Endorsement itaathiri usajili wa wachezaji wa kigeni kutokana na hali ya kisiasa nchini Uingereza wakati huu ambao wanapambana kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya [Brexit].
Pamoja na yote, kinachosubiriwa kwa Diallo ni kibali cha kufanyakazi nchini Uingereza na muda muafaka wa dirisha la usajili kufunguliwa ili usajili wake ukamilike na aungane na wachezaji wengine wa United.

Bado haijajulikana kama Diallo atacheza kwenye kikosi cha wakubwa au atakwenda U23 kama ilivyo kwa Facundo Pellistri. Kwa hali ilivyo, Diallo hawezi kucheza mashindao ya vijana ya FA Cup na U23 hawana mechi mpaka Januari 18.
Kwa hali hiyo, Ole Gunnar Solksjaer anawezakumpatia nafasi Amad Diallo kwenye benchi lake kwenye timu ya wakubwa kwani anauzoefu wa kucheza mechi za Serie A na Ligi ya Mabingwa ambazo zote alicheza kwa muda mfupi kabla ya kutimkia United.
Huenda mchezo wa mwisho kwa Diallo kuitumikia Atalanta utakuwa dhidi ya Bologna kesho – Jumatano na baada ya hapo ataendelea na taratibu za kukamilisha usajili na United.
Diallo atakuwa anakamilisha idadi ya wachezaji 5 waliosajiliwa mwezi Julai ikiwa ni pamoja na Donny van de Beek, Edinson Cavani, Alex Telles na Facundo Pellistri.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???
Adelta
Amad Yuko vizuri
Dorophina
Karibu united amad
Ernest Kimeru
Litakuwa Deal zuri kwa Amad Diallo
Sarah
Amar Yuko vizuri
Shakila mrope
Amani kribu chaman united
aisha
Safi sana amad
Saupha mohamed
Jambo zuri
Asia Abdy
Good
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa poa man U wakimpata kiungo uyo
David Pere
Kutokana na utaratibu mpya ambao nchi ya Uingereza umeueka na utaanza kufanya kazi kuanzia Januari 1, kulikuwa na mashaka kama usajili wa Amad Diallo utakamilika kabla ya makubaliano ya Governing Body Endorsement kuanza kutumika.
Fatina mfingi
Itakuwa powah sana
farida ahmad
Habari njema kwa mashabiki wa man United
Mariam mtandama
Vizur
Issa
Diallo anatakiwa aonyeshe makali yake akiwa na united
Mnongane JR
Fundi wa mpira karibu man utd#meridianbettz#
Hopemwaikuka
Karibu chama la wajanja
Tatu
Karibu
warda
Sio mbaya anaweza kutubusti busti