Mchezaji wa timu ya Manchester United Amad Diallo yuko njiani kumalizia uhamisho wa kuahamia kwenye klabu ya Rangers kabla ya dirisha la mwezi January kufungwa siku ya Jumatatu usiku.
Mkataba wa mkopo wa kinda huyo hautahusisha kifungu cha klabu ya Rangers kuweza kumnunua mwishoni mwa msimu, Amad Diallo anakwenda kwenye klabu hiyo ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara nyingi ili kupata uzoefu wa kutosha.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa Amad Diallo angepelekwa kwa mkopo kwenye klabu zinazoshiriki ligi ya championship nchini Uingereza, huku klabu ya Derby Country ilionesha hali ya kuhitaji huduma yake lakini kocha wa timu hiyo Wayne Rooney alitupilia mbali uwezekano huo.
Amad ameicheze timu ya wakubwa michezo tisa tu mpaka sasa na kufunga goli moja tu, endapo usajiri wake utafanikiwa basi atapata nafasi ya kucheza michuano ya Europa League ngazi ya mtoano akiiwakilia klabu ya kutoka nchini Scotland mwezi ujao.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.