Amorim Matumaini Kibao kwa Mount

Kocha mpya wa klabu ya Manchester United Ruben Amorim ameonekana kua na matumaini na kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount ambaye amekua akisumbuliwa na majeraha.

Ruben Amorim amesema anavutiw ana Mount na anamuona kama mchezaji ambaye ana hamu kwelikweli ya kurejea kwenye ubora wake ambao amekua nao baada ya kusumbuliwa mara kwa mara na yeye binafsi ameweka wazi anavutiwa na ambacho anakiona kwa mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea.amorimMason Mount… lazima nikwambie, nampenda sana huyo kijana. Ukiangalia machoni mwake, utaona jinsi anavyotaka hili kwa dhati. Hii ndiyo kitu muhimu zaidi.”

“Alicheza kwenye mfumo huu, kwa hivyo ni kamili kwake… Nina nafasi mbili kwa Mason Mount, kwa hivyo anapaswa kuwa na furaha kubwa!”

Mason Mount amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ndani ya klabu hiyo tangu ajiunge nayo mwaka 2023 na kushindwa kuonesha makali yake, Lakini inaonekana kocha Amorim amekua na imani na kiungo huyo huku akisisitiza itakua rahisi kwa kiungo kwakua ameshwahi kucheza kwenye mfumo anaoutumia kipindi akiwa Chelsea chini ya Thomas Tuchel.

Acha ujumbe