Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Morocco Sofyan Amrabat ameonekana katika kiwanja cha mazoezi ya klabu hiyo kinachofahamika kama Carrington mapema leo.

Amrabat ameonekana na kundi la wachezaji wenzake wakifanya mazoezi kwa pamoja leo, Huku ikiwa ni baada ya kuripotiwa kupata majeraha wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Morocco.AmrabatKiungo huyo wa kimataifa wa Morocco alizua hofu klabuni hapo baada ya kuripotiwa kupata maumivu ya mgongo wakati akiitumikia timu ya taifa ya Morocco, Lakini kuonekana kwake leo mazoezini kumeibua faraja kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Klabu ya Manchester United ilipokea taarifa mbaya katika michezo ya kimataifa iliyokua inaendelea kwani kiungo wake raia wa kimataifa wa Brazil Casemiro alipata majeraha wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Brazil.AmrabatBaada ya kiungo Sofyan Amrabat mazoezini ni wazi sasa yeye ndio atakwenda kuvaa viatu vya Casemiro ambaye ampeta majeraha, Kwani beki wa kushoto aliyepo klabuni hapo kwa mkopo Sergio Reguilon amerejea pia hivo kiungo huyo hatatumika tena kwenye nafasi ya beki wa kushoto.

 



JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa