Klabu ya Manchester United imeendelea kutafuta wachezaji ili kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao na sasa wamehamia kwa kiungo wa kimataifa wa Morocco anayekipiga Fiorentina na Italia Sofyan Amrabat.
Manchester United wanamuhitaji Sofyan Amrabat kama sehemu ya kukiongezea nguvu kikosi hicho kwenye eneo la katikati ya uwanja, Kwani mpaka sasa wameshafanikiwa kusajili mchezaji mmoja kwenye eneo lakini wanahitaji kusajili mchezaji mwingine.Mkurugenzi mkuu wa Fiorentina Barone amesema amesikia taarifa za klabu ya Manchester United kumuhitaji mchezaji wao, Lakini akisema mpaka sasa hawajapokea ofa yeyote kutoka kwa wababe hao wa soka kutoka nchini Uingereza.
Man United wanamuona Amrabat kama kiungo mzuri mbadala wa kiungo wao wa ulinzi Carlos Casemiro, Hivo wakimsajili mchezaji huyo watakua wameweza kuboresha kikosi chao kwa kiwango kikubwa kwakua watakua wameongeza ubora kikosini.Sofyan Amrabat amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya kikosi cha Fiorentina pamoja na timu ya taifa ya Morocco ambapo alikua mchezaji muhimu wakati timu hiyo inatinga hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka jana nchini Qatar.