Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amethibitisha kwa kusema kuwa mshambuliaji wake Kareem Benzema atalazimika kukaa nje kwenye mchezo wa Derby wa leo dhidi ya Atletico Madrid ambapo utapigwa majira ya saa 22:00 usiku.

 

Ancelotti Athibitisha Benzema Kuikosa Derby

 

Mchezaji huyo wa timu ya Ufaransa alipata jeraha la goti kwenye mchezo wa klabu Bingwa ambapo walikuwa wakicheza dhidi ya Celtic na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, ambapo Benzema alitoka mapema nje  katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao walikuwa ugenini.

Ancelotti hapo awali alisema kuwa Benzema kuwa fiti kwaajili ya mchezo wa Derby na Atletico wikiendi hii, Lakini pia alitahadharisha wakati huo kwa kusema ikiwa hatapona pia, hatakuwepo kwa mapumziko yajayo ya Kimataifa.

Huku Benzema akiwa hayupo kwenye kikosi cha Didier Deschamps cha Les Bleus wiki hii, ilionekana kutocheza Wanda Metropolitana, jambo ambalo Carlo alithibitisha katika mkutano wake na waandishi wa habari akisema. Sisemi ni nani atakayecheza mbele , Benzema hatakuwepo. “Ameanza kufanya mazoezi binafsi na atakuwa tayari baada ya mapumziko ya Kimataifa”

 

Ancelotti Athibitisha Benzema Kuikosa Derby

Ancelotti alizungumzia pia kuhusu maoni ya hivi juzi yenye utata kutoka kwa Pedro Bravo ambaye ni wakala mkuu nchini Hispania kuhusu,  Vinicius Junior juu ushangiliaji wake wa Samba Dansi ambao Pedro alisema kuwa unahusishwa na ubaguzi wa rangi, lakini baadae wakala huyo aliomba msamaha na kusema alitumia neno hilo vibaya.

Carlo alisema kuwa “Ni jambo ambalo hatuligusii kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, haya ni masuala ambayo hayajadiliwi kwenye vymba vya kubadilishia nguo, huwa tunazungumza kuhusu soka”

“Ubaguzi wa rangi ni jambo moja na kinachotokea kwenye soka ni kitu kingine. Hatujagusia suala hili la ubaguzi wa rangi kwasababu mchezaji amejibu vizuri sana.”

 

Ancelotti Athibitisha Benzema Kuikosa Derby

Na baadae Ancelotti  aliulizwa kama ameongea na Vini kuhusu suala hilo lakini alijibu kuwa yeye si baba yake wala ndugu yake yeye ni kocha wake na mchezaji huyo anacheza kwa furaha na anafuraha. Madrid mpaka sasa ndio timu pekee pale Laliga iliyoshinda mechi zake zote bila hata ya kutoa sare katika mashindano yote na leo watakuwa wakimenyana na Atletico Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa