Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema hawana hofu na Manchester City baada ya kupangwa kukutana nao katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Droo ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya ilichezeshwa leo na Real Madrid watakutana na Manchester City katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo itakayopigwa hapo baadae mwezi April.Kocha Ancelotti anasema hafikirii kama wachezaji wako wanaihofia Man City baada ya kupangwa nao kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, Huku akisisitiza kua wako tayari kupambana kwakua wanajiamini vya kutosha.
Ancelotti huyo pia ameongelea wachezaji wake ambao walikua na majeraha kwa muda mrefu ambao ni beki Eder Militao na golikipa namba moja Thibaut Courtois ambao wameshaanza mazoezi na timu akisema watakua sehemu ya kikosi kwenye mchezo huo.Real Madrid dhidi ya Manchester City wanakutana kwa mara ya tatu mfululizo ndani ya miaka mitatu mwaka 2022 wakifanikiwa kushinda Madrid na kwenda fainali, Huku 2023 ikawa zamu ya Man City kushinda na kwenda fainali inasubiriwa awamu hii nani atafanikiwa kushinda na kwenda hatua ya nusu fainali.