Ancelotti Afunguka Kumuweka Benchi Hazard

Carlo Ancelotti amefunguka juu ya Eden Hazard kufuatia kukosekana dimbani kwa Mbelgiji huyo hivi karibuni.

Hazard aliwekwa benchi kwa dakika 90 wakati Real Madrid walipopata ushindi dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye Ligi ya Mabingwa Jumatano.

Winga huyo mwenye thamani ya zaidi ya Euro milioni 100 amekuwa akihudhuria benchi mara kibao chini ya Ancelotti, ambaye amekiri kwamba Mbelgiji huyo si chaguo la kwanza kwake kwa sasa.

Jumatano usiku pia Hazard aliachwa benchi licha ya winga wa kwanza wa kulia Rodrygo kuwa hayupo.

Ancelotti Afunguka Kumuweka Benchi Hazard

Badala yake, Lucas Vazquez alichaguliwa kucheza na Hazard aliachwa benchi kwa dakika zote 90 , wakati Ancelotti akibadilisha wachezaji wawili tu kati ya watano.

Hii ni changamoto nyingine kwa nyota wa zamani wa Chelsea, ambaye alitarajiwa kuwa supastaa pale Santiago Bernabeu.

Licha ya Ancelotti kukiri kwamba Hazard anahitaji mda wa kucheza ili arejee kwenye ubora, anadai kuwa hilo linaweza kufanyika wakati wowote.

“Hazard yuko tayari kucheza, ingekuwa leo au inaweza kuwa Jumamosi. Ni kweli kwamba anahitaji mda wa kucheza kuwa katika hali yake ya ubora. Nimefikiria kumuweka, lakini kimkakati, niliweka winga.” -Ancelotti


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe