Ancelotti Aelezea Sababu ya Kumuacha Bale

Carlo Ancelotti ameeleza sababu ya kukosekana kwa Gareth Bale kwenye kikosi cha Real Madrid cha Clasico siku ya Jumapili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales alipewa nafasi ya kuanza dhidi ya Villarreal, na alifanya vizuri kwenye mechi hii, lakini tangu wakati huo, amekuwa kama mchezaji wa akiba bila kutumiwa.

Japokuwa Jumapili, Ancelotti angeweza kuhakikisha Bale anakuwepo kikosini, wakati wakimkosa Karim Benzema lakini haikuwa hivyo.

Hiyo haimaanishi kwamba Muitaliano huyo angemtumia Bale, baada ya kumpuuza mara nyingi zaidi kwa miezi kadhaa, lakini chaguo hili lingekuwa muhimu kwa wakati huu.

Kulikuwa na matarajio makubwa kutroka benchi ya Real Madrid, ilishangaza kuona mkongwe huyo wa Wales akikosekana kwenye kikosi kizima cha Los Blancos dhidi ya Barcelona, wakikubali kichapo cha 4-0.

Lakini Ancelotti ameelezea kuwa alikuwa na shida ya kiafya ambayo pia inaweza kumuweka kwenye wasi wasi wa kukosekana kwenye kikosi cha taifa.

“Sijui nini kitatokea kwa Wales, lakini [Gareth Bale] hakuwa sawa.” – Carlo Ancelotti


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe