Ancelotti:Rodrygo Kaacha Uanafunzi.

Rodrygo ni mshambuliaji mzuri, Carlo Ancelotti amemsifu mchezaji huyo baada ya kufunga bao kwenye mchezoo dhidi ya Betis.

Ancelotti:Rodrygo Kaacha Uanafunzi.

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti alisema kuwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amejidhihirisha ubora wake baada ya kumuona akifunga bao la ushindi katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Betis.

Ancelotti:Rodrygo Kaacha Uanafunzi.

Rodrygo alihakikisha Real Madrid wanadumisha mwanzo wao mzuri wa msimu wa La Liga, kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Real Betis 2-1 katika dimba la Santiago Bernabeu Jumamosi.

Ancelotti:Rodrygo Kaacha Uanafunzi.

Vinicius Junior alianza kufunga bao baada ya dakika tisa pekee, lakini Real Betis wakarudi mchezoni wakati Sergio Canales aliposawazisha kipindi cha kwanza.

“Ni mshambuliaji mzuri kwangu kwa sababu anaweza kucheza katika nafasi zote,” Ancelotti alisema kuhusu Rodrygo baada ya mechi. “Yeye ni mwepesi, mwerevu bila mpira, anafanya kazi vizuri katika hali ya mtu mmoja mmoja. Uanafunzi wake umekwisha na sasa ni mchezaji wa Real Madrid kwa nia na madhumuni yote.”

Ancelotti:Rodrygo Kaacha Uanafunzi.

Acha ujumbe