Kocha wa klabu ya Real Madrid na mabingwa watetezi wa ulaya Carlo Anchelotti amekisifu kikosi chake cha sasa ndani ya klabu hiyo na kusema ni miongoni mwa vikosi bora vya muda wote kama sio bora.anchelottiKocha huyo ambaye ana rekodi ya kua kocha wa kwanza kubeba taji la ligi ya mabingw ulaya mara nne ikiwa haijawahi kufanywa hivo na kocha mwigine yeyote amezungumza jambo hilo baada ya mchezo kati yao na klabu ya Sevilla kumalizika na kupata ushindi katika mchezo huo.

Kocha Anchelotti ambae amewahi kufundisha vikosi vingi bora lakini amefunguka kua anadhani kikosi chake cha sasa ndani ya klabu hiyo ni miongoni vya vikosi bora zaidi kuwahi kufundisha kama sio ndo bora zaidi kuliko vingine.

Ikumbukwe Anchelotti amewahi kufundisha magwiji kama Zidane, Ronaldo de Lima, Cristiano Ronaldo, Paulo Maldini, Roberto Lewandwski, pamoja Ricardo Kaka lakini amekisifu kikosi chake cha sasa ndani ya Real Madrid.anchelottiKutoka na kauli ya kocha huyo imeibua mijadala tofauti tofauti wengi wakionesha kutokukubaliana na mwalimu huyo na kuamini labda amezungumza hivo kama sehemu ya kuwapa motisha wachezaji waliopo klabuni hapo lakini kiuhalisia wakiamini kocha huyo amewahi kua na kikosi bora kuliko hichi cha sasa cha Real Madrid.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa